Monday, August 6, 2012

NEWZ NEW 2012


NDOTO ZA OLIMPIKI KATIKA PICHA


Mkuu wa Olimpik Morocco kukamatwa

 
Jenerali Housni Benslimane atakikana na polisi Ufaransa
Jaji mmoja nchini Ufaransa amewaomba polisi wa Uingereza wamkamate kiongozi wa ujumbe wa Olimpik wa Morocco ambaye kwa sasa yuko jijini London.
Kiongozi huyo wa Olimpiki Jenerali Housni Benslimane,anadaiwa kuhusika na kutoweka kwa kiongozi wa upinzani wa Morocco Bwana Mehdi Ben Barka.
Mwanasiasa huyo wa upinzani wa Morocco wa alitoweka mwaka 1965 akiwa Ufaransa.
Jaji Patrick Ramael tangu mwaka wa 2007 amekuwa akitaka Housni Benslimane akamatwe.
Jaji huyo amekuwa akitaka kiongozi huyo wa Olimpik na wanajeshi watatu wa zamani wa Morocco wahijiwe kutokana na kutekwa nyara kwa Bwana Ben Barka mjini Paris.
Lakini ubalozi wa Moroccan mjini London unasema kuwa Jenerali Benslimane alikuwa jijini humo wiki iliyopita lakini ameshaondoka.
Ingawa Jaji Ramael alitoa waranta yakutaka kiongozi huyo wa Olimpiki akamatwe miaka saba iliyopia lakini haitambuliki kwa sababu hadi sasa polisi wa kimataifa Iterpol na wakuu wa mashitaka nchini Ufaransa bado hawajaikubali.


Mashambulizi makali yatokea Ivory Coast


Wanajeshi wa Ivory Coast waliouawa
Majambazi waliokuwa wamejihami wameshambulia kambi ya kijeshi mjini Abidjan, mji mkuu wa Ivory Coast na kuwaua takriban wanajeshi sita.
Wenyeji walielezea kusikia milio ya risasi usiku kucha katika mtaa wa Riviera. Idadi kubwa ya wanajeshi wakiwemo walinzi wa amani wa umoja wamataifa, wamepelekwa katika eneo hilo ingawa sasa maafisa wakuu wanasema kuwa hali imeweza kudhibitiwa.
Mji huo ulishuhudia mapambano makali, mwaka jana wakati wa mvutano wa kisiasa ambao ulitokea baada ya matokeo ya uchaguzi ambayo yalizua utata mkubwa.
Mnamo siku ya Jumapili, wapiganaji waliokuwa wamejihami walishambulia kizuizi cha jeshi barabarani katika eneo la Yopougon mashariki mwa Ivory Coast pamoja na kituo cha polisi na kuwaua wanajeshi watano katika kambi ndogo ya kijeshi mjini Abidjan.
Wapiganaji hao walivalia sare za kijeshi na kutumia silaha nzito nzito japo hawakuweza kutambuliwa.
Milio ya risasi pia ilisikika mwishoni mwa wiki katika eneo la Abengourou mashariki mwa nchi na sababu ya shambulio aijajulikana.
Shambulio hilo lilitokea katika wilaya ya Yopougon ambayo inaaminiwa kuwa mojawapo ya wilaya zilizoshambuliwa zaidi na waasi wakati wa machafuko na hatimaye ushindani wa uongozi wa Abidjan kufuatia matokeo yaliyozua utata wa uchaguzi wa urais mwaka jana.
Maiti wanne walionekana katika mlango wa jengo moja katika kambi ya jeshi ya Akouedo huku damu ikionekana imetapakaa kwenye sakafu na hata kwenye ukuta. Mlango huo ulikuwa umevunjwa. Miili mingine miwili ilipatikana katika lango lengine kubwa.

Keita aondoka Barcelona

 9 Julai, 2012 - Saa 10:06 GMT
Mchezaji wa kiungo wa Mali Seydou Keita amekihama klabu cha Barcelona baada ya kukichezea kwa miaka minne.
Seydou Keita na wenzake wakisheherekea ushindi
Katika muda huo wa miaka minne, Keita aliisaidia Barcelona kuzoa jumla ya vikombe 14.
Wakati wakithibitisha kuondoka kwa mwamba huyo, Barca walimishukuru Seydou Keita kwa juhudi zake za kuletea klabu hicho cha Uhispania mafanikio na vile vile wakamtakia kila lakheri anakokwenda.
Kwa wakati huu kuna fununu kwamba mchezaji huyo wa Mali huenda anahamia klabu kimoja cha Uchina, Dalian Aerbin
Ikiwa hatiamae ataishia China basi Keita hatakuwa mchezaji wa kwanza kutoka bara la Afrika kufanya hivyo.
Majuzi nahodha wa timu ya Ivory Coast Didier Drogba aliwafuata Frederic Kanoute na Yakubu Aiyegbeni wa Nigeria kujiunga na timu za ligi kuu ya China.
Keita, mwenye umri wa 32, alijiunga na Barcelona mwaka 2008 kutoka Sevilla akiwa ni mchezaji wakwanza kabisa ambaye Pep Guardiola alimsajili mara tu alipochukuwa uongozi wa Barca.
Kabla ya hapo mchezaji huyo alikuwa Olympic Marseille, Lorient na Lens zote za Ufaransa na ndio baadaye akahima Seville ya Uhispania.
Keita amehama baada ya Guardiola luondoka kama Meneja wa Barcelona na mahali pake kuchukuliwa na aliyekuwa naibu wake Tito Vilanova


Ivory Coast violence: Abidjan army attack kills seven

A patrol of the Ivory Coast Republican Force (FRCI) ride to a search operation on August 6, 2012 in Bingerville, a town near Abidjan. The army is conducting extra patrols looking for the 

Rebuilding Ivory Coast

At least six soldiers have been killed in an attack by gunmen on an army base in Ivory Coast's main city, Abidjan.
One assailant was also killed in the gun battle which lasted several hours in the Riviera district of Abidjan.
This follows the shooting of five soldiers on Sunday in an attack on a police station and an army checkpoint in Yopougon to the east of the city.
It is not clear who was behind the attack. Ivory Coast is recovering from months of unrest after a disputed poll.
The two attacks are said to be the biggest in Abidjan since former President Laurent Gbagbo was ousted in April 2011.
The BBC's John James in Abidjan says there is a gory scene at the Akouedo military camp, with bodies lying on the ground and blood spattered over the walls.
Corp Ousmane Kone, who took part in the fighting, told Reuters news agency that the attackers had made off with guns.
"They took lots of weapons, loaded them in a truck and drove off with them. They took AK-47s [automatic rifles], machine guns and rocket-propelled grenades," he said.



Usain Bolt, mwanariadha kutoka Jamaica na anatazamiwa kufanya maajabu 2012

No comments:

Post a Comment