SHUGHULI YA KUTAFUTA MAITI ZANZIBAR
Meli ya Mv SKAGIT ikimalizikia kuzama jana katika eneo la Chumbe Zanzibar
Shughuli
ya kutafuta maiti kwenye ajali ya meli iliyozama nchini Zanzibar
ilianza leo mapema huku watu miamoja wakiwa bado hawajapatikana baada
meli iliyokuwa inaelekea kisiwani Zanziabr kuzama eneo la Chumbe.
Meli hiyo ilitoka Dar Es Salam jana mcahan kuelekea kisiwani ikiwa imebeba watu miambili tisini.
Hadi kufikia sasa maiti 31 wamepatikana huku watu zaidi ya 150 wakiokolewa.
Msemaji wa polisi nchini Zanzibar
aliambia shirika la habari la AFP kuwa kwa sasa kuna hofu ya
kutopatikana manusura wowote waliokuwa katika meli hiyo ya MV Skagit
"shughuli ya kuwatafuta manusura
na maiti inaendelea lakini kwa sasa ni vigumu kwa kweli kupata
manusura." alinukuliwa akisema msemamji huyo wa polisi.
No comments:
Post a Comment