Sunday, August 5, 2012

FARASI , JEMBE MRISHO NGASA ATUA CHAMA KUBWA SIMBA


 Aliyekuwa mchezaji wa Azam,Mrisho Ngassa akiwa ameegemea gari yake aliyokabidhiwa jana mara baada ya kuwasili katika ufukwe wa Coco Beach kwa kuungana na wachezaji wenzake wa Simba baada ya maridhiano ya Azam,Simba na yeye kumalizika

BEYONCE KUSHOOT VIDEO YA WIMBO WAKE WA "I WAS HERE" SIKU YA WORLD HUMANITARIAN DAY.



Mwanadadiva mwenye mtoto mmoja muite mama Ivy mke wa mkali wa kwenye ngoma ya Ortis Jay z akiwa na Boss wa Good Music Kanye West mwanamama Beyonce, amejitolea sauti yake iliyobarikiwa kwenye kitu cha maana. Beyonce ametangaza kufanya video ya ngoma ya “I was Here” kwa heshima ya World Humanitarian Day, siku hiyo wakati akiperform watu watakaoonekana ndo itaonekana kwenye video yake hiyo.
 Diva huyo amejiunga na shirika la United Nations & Humanitarian Aid Organization kwa ajili ya kuzindua kampeni ya kusherekea kazi za kujitolea zinazofanywa na watu mbalimbali na kuwapa moyo watu duniani kote kufanya mambo mema kwa watu wengine ambao wako kwenye matatizo. Video itafanywa na kampuni ya Ridley Scott & Associate na madirectors wakali kama Kenzo Digital na Sophie Muller. Kampeni hiyo inalengo la kufikia watu bilioni 1 na ujumbe mmoja wakati wa uzinduzi siku hiyo.

ANDRE 3000 KUDIRECT VIDEO 16 KUTOKA KATIKA ALBUM YA GOD FORGIVES, I DON’T YA ROZAY.


Mkali aliyerikishwa kwenye ngoma ya Green light ya John Legend member wa OutKast akadrop bars za ukweli  homie Andre 3000 sio tu kwamba amealikwa auzee sura kwenye video!!  no pia anadirect video 16 za Bawse Rozay  kutoka kwenye album ya “God Forgives, I don’t”
“3000 kwa sasa bado anaongezea mawazo mapya kwenye video hizo ili aweze kufanya video kali” alisema Rozay  ambae ni Boss wa Maybach Music wakati akipiga stories na MTV News kwenye RapFix Live Jumatano iliyopita.
Rozay mpaka sasa ameshaachia ngoma nne kutoka kwenye album hiyo na anayo mipango ya kuachia nyingine zaidi. Atafanya video za ngoma zote ambazo zinapatikana kwenye album yake.

Wednesday, August 1, 2012

HUYU NDIO MTOTO WA KYSHER


Mtoto wa msanii kysher, daaah jina lake gumu hilo ngoja nilikumbuke heheeee...eheeeeeeeeee nimekumbuka anaitwa Jamkey au Adnan....cute cute 

EPIC BSS YAWASHA MOTO VIWANJA VYA COCO BEACH HII



CHRISTOPHER KAJA NA SWAGGA YAKE YA KIPEKEE 

MASHINDANO ya kusaka vipaji kwa washiriki wa Bongo Star Search (EBSS) kwa Mkoa wa Dar es Salaam
yameanza rasmi katika fukwe za Coco Beach.

Ikilinganishwa na mikoa mingine ambapo usaili ulichukua siku mbili, usaili wa Dar es Salaam utachukua
siku tatu na mpaka sasa vijana wengi wamejitokeza katika usaili huo.

Akizungumzia usaili wa Dar es Salaam Jaji Mkuu wa EBSS 2012, Ritha Paulsen alisema kutokana na
historia ya mkoa huu katika usaili wake kuhudhuriwa na watu wengi zaidi, hivyo anategemea ushindani
kuwa mkubwa zaidi.

“Nashukuru Mungu kuwa tumemaliza salama mikoani na kuanza rasmi Dar es Salaam kwa ajili ya
kufunga kabisa pazia la ushiriki wa EBSS,” alisema Ritha.

Ritha aliongeza kuwa mapema mwezi ujao washiriki wataanza kuingia kambini kwa ajili ya mashindano
hayo na kuongeza kuwa EBSS kwa mwaka huu itakuwa ni bora zaidi.

Epic Bongo Star Search 2012 mshindi ataondoka na shilingi milioni 50 kutoka kwa wadhamini wakuu
ZANTEL. Umri wa kushiriki ni kuanzia miaka 16. Fomu zinaendelea kutolewa bure katika ofisi za Zantel,
maduka ya Zantel na Coco Beach pia.





MI SINA TATIZO NA MTUUUUUUU

CAESAR DANIEL, LEON COETZER NA SWEDE WA BENCHMARK WAKIWAHOJI WASHIRIKI


MSANII NA MTOTO WA MITAANI BALAJA ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUTUHUMIWA KUIBA


Leo hii, maeneo ya manyanya, mtoto wa mitaani ambae pia alishawahi kurekodi wimbo (maumivu) pamoja na video yake, chini ya msaada wa fish crab producer Lamar, amepigwa nusu ya kufa na wananchi baada ya kutuhumiwa kumuibia mtu asiyejulikana aliekuwa kituo cha basi, "watu wamempiga sana, alikua keshaanza kutoka damu mdomoni, mi nimefika pale ndio wakaacha kumpiga" amesema lamar ambae alikua eneo la tukio
Balaja anatokea kahama mkoani shinyanga, mara nyingi amekuwa akiomba nauli ya kurudi kwao ambapo anadai kuishi na bibi yake, lakini kila akidakiswa nauli, kesho unamkuta tena mitaani..siku kadhaa zilizopita nilipost habari kuhusu sababu za Lamar kuacha kufanya nae kazi..pitia story za nyuma ucheki na video ya wimbo wake

JAGUAR AKANA KUTUMA TWEETS ZA CHUKI DHIDI YA PREZZO

 leo hii kupitia mtandao wa twitter, kumekuwa na vurugu za maneno katika ya anaejiita @JaguarKenya na fans wa Prezzo, baada ya kutweet maneno ya chuki dhidi ya Prezzo, na kuwaomba fans wake wasimpigie kura, na hata kudiriki kusema kuwa, kama PREZZO atashinda basi yeye atahamia Uganda. hehehe 
JAGUAR HATE
hata hivyo Fans hao hawakukaa kimya na kutiririka, huku asilimia kubwa  ikimponda mzee wa kigeugeu kama ilivyo hapo chini 

Hata hivyo kupitia mtandao wa ghafla, Jaguar amekana kutuma tweets hizo kwa kusema kuwa yeye ana account ya facebook peke yake,na hiyo account si yake na wala hayuko agaisnt Prezzo bali anatoa support kama Mkenya, so tweetz hizo tupa kule.



RAILA ODINGA AHAMASISHA WAKENYA KUMPIGIA KURA PREZZO


King wa bling hatimae ameingia katika fainali za Bigbrother zitakazo fanyika jumapili ya wikii hii, show imebakiwa na washiriki sita kwa sasa walioingia fainali ambao ni , Prezzo, Lady May, Keagan, Wati na Talia.
kwa mtazamo wa watu wengi inaonekana Prezzo yuko karibu sana na dola za kimarekani 300,000 amabayo ndio atakazopata mshindi wiki hii..
katika nchi 15 zinazohusika katika kupiga kura, kila kura ya nchi hizo itahesabika kama kura moja kila nchi itakayopiga kura basi kura itahesabiwa kama ni moja, kwahiyo mwenye kupata kura chache, atakosa chance ya kurudi na mkwanja.
kampeni ya kupigia kura prezzo imeonekana kuongezeka speed baada ya waziri mkuu kenya kutweet 


SIKILIZA U HEEEEARD!!! YA LEO JUMATANO TAREHE 1/8/2012.

MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE DHIDI YA TUHUMA ZA RUSHWA HUSUSAN KUELEKEA KATIKA KUPITISHA BAJETI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI



Ndugu Waandishi,
Nalazimika kukutana nanyi kutoa maelezo juu ya tuhuma zenye shinikizo la kisiasa zinazoelekezwa kwangu binafsi kwamba hata mimi nimeshiriki katika vitendo vya rushwa, kwa nafasi yangu kama Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma. Taarifa hizo, kama kawaida ya uzushi mwingine wowote  zimesambazwa kimkakati na kwa kasi kubwa kiasi cha kuukanganya umma.
Nafahamu nabeba dhamana kubwa ya uongozi, taswira yangu ya uongozi daima imeakisi njozi na matumaini ya wananchi wa Kigoma Kaskazini, wananchi wanyonge na vijana kote nchini bila kujali itikadi zao za kisiasa, jinsia zao, makabila yao na rika zao. Hivyo, nawajibika kupitia kwenu kuwatoa hofu juu ya hisia potofu zinazopandikizwa kwao na wale wasiopenda kuona baadhi yetu tukiwaunganisha na kuwasemea watanzania wasio na sauti, dhidi ya vitendo vya hujuma na vyenye dhamira ovu kwa taifa.
Mkakati huo wa kuniunganisha na baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wanaotuhumiwa kwa kupokea Rushwa unatekelezwa kwa njia zifuatazo:
  1.   Kumekuwa na kauli za watendaji wa serikali ambao wamekuwa wakizieneza na hususan kutoa taswira kwamba baadhi ya kauli zangu zinatokana na ushawishi wa rushwa;
  2.   Kuna taarifa ambazo zimeandikwa tena katika kurasa za mbele za baadhi ya vyombo vya habari  zikidai ’’Zitto kitanzini’’ ama ’’Zitto sawa na popo nundu’’  zikiashiria kwamba na mimi ni mla rushwa; na
  3.   Waandishi wa habari na jamii kwa ujumla wamefikia kuaminishwa habari hizi kiasi cha wengine kuuliza kwa nini Mhe. Zitto Kabwe hakutajwa katika orodha iliyotolewa na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani.
Ndugu Waandishi,
Naomba kutoa ufafanuzi wa hicho kinachoelezwa kwamba nina ushiriki katika masuala ya rushwa hususan kwenye masuala yanayohusu sekta ya Nishati na Madini:-
  1. Mara baada ya bodi ya Wakurugenzi ya  Shirika la Usambazaji wa Umeme Tanzania (TANESCO) chini ya Uenyekiti wake Meja Jenerali Mstaafu Robert Mboma kutangaza kwamba imemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Nd. William Mhando ili kupisha uchunguzi wa baadhi ya vitendo/mwenendo wake, Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) ambayo mimi ni Mwenyekiti wake ilimuandikia Mhe. Spika kumuomba aridhie ili Kamati iweze kuwaita Bodi ya TANESCO, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali  (CAG) na pia Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kujiridhisha na tuhuma zote zinazotajwa zinafanyiwa uchunguzi wa kina na hatua kuchukuliwa;
  2. Kamati ya POAC ninayoiongoza ilimuomba Mhe. Spika kuwaita wahusika tajwa kwa kuwa zilikuwapo tetesi kuwa kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi huyo siku chache kabla ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kulikuwa na lengo la kufunika ’madudu’ makubwa zaidi kwa kulichagiza Bunge na tukio hilo dogo, mkakati ambao naona umefanikiwa sana. Isitoshe, Kamati kutaka kujiridhisha na hatua za Bodi ni sehemu ya msingi ya utekelezaji wa majukumu ya Kamati yaliyowekwa kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge na pia Shirika la TANESCO ni moja kati ya mashirika ambayo yanawajibika kwetu kwa hesabu zake na pia ufanisi wake kwa ujumla. Tumefanya hivyo pia katika mashirika mengine, hili la TANESCO sio tukio la kipekee;
  3. Kitendo hiki cha halali na kwa mujibu wa Kanuni kilichofanywa na Kamati yangu  kimetafsiriwa kwa makusudi na baadhi ya watu kwamba ni ishara ya kuwa sisi au zaidi kwamba mimi nina maslahi binafsi na TANESCO na hususan Mkurugenzi wake Injinia Mhando, ndio maana tumetaka maelezo ya Bodi. Ukweli kwamba Kamati ya POAC tumewaita pia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu (CAG) na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kwa jambo hilo hilo umefichwa kwa makusudi!
  4. Baada ya  tukio hilo, nikiwa hapa Dodoma, mwandishi wa habari wa gazeti moja alinifuata akiniambia kuwa wamekutana na Mhe. Waziri Mhongo na Katibu Mkuu wake, Nd. Eliachim Maswi hapa hapa Bungeni na wamewaambia kuwa mimi nimepewa rushwa. Hakutaja nimepewa rushwa na nani, kiasi gani na wala kwa lengo gani!
  5. Nimejaribu kumtafuta kwa simu Mhe. Waziri Mhongo na Katibu Mkuu wake ili wanipe ufafanuzi juu ya mimi na Kamati ya POAC kuhusishwa na tuhuma hizi bila mafanikio, hali ambayo inaniondolea mashaka juu ya ushiriki wao katika kueneza au kuthibitisha uvumi huo. Najaribu sana kujizuia kutokuwa na mashaka na ushiriki wao huo ikizingatiwa uzito na taswira ya nafasi zao katika jamii, lakini wameshindwa kunidhihirishia tofauti.
Sasa naomba kutoa ufafanuzi rasmi kuhusu mlolongo wa matukio hayo tajwa ambayo yanatumiwa na baadhi ya wanasiasa kuonesha kwamba eti nimehusika na vitendo vya rushwa.
  1. Binafsi sijawahi kuwa na mawasiliano ya aina yeyote na uongozi wa TANESCO kushawishiwa juu ya hatua ambazo POAC ndio imezichukua za kutaka kujiridhisha juu ya utaratibu uliotumika. Ieleweke wazi kabisa kuwa, hakuna wakati wowote, popote ambapo mimi binafsi au Kamati yetu imekataa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO kuchunguzwa kwa tuhuma zozote. Ambacho tumesisitiza wakati wote ni ufuatwaji wa taratibu, kanuni na sheria, hili nitalisimamia iwe masika au kiangazi;
  1. Ni kwa sababu hiyo, na kwa kujiamini kabisa nimeunga mkono suala la tuhuma za rushwa zinazotajwa zichunguzwe na Kamati ya Haki, Maadili na  Madaraka  ya  Bunge kwa kina;
  1. Nimekwenda mbali zaidi kukiomba chama changu CHADEMA kifanye pia uchunguzi na tathmini yake kwa kina kujiridhisha na tuhuma hizo;
  1. Natumia fursa hii pia kuomba vyombo vya Dola vichunguze tuhuma hizo kwa nafasi yake ili kuweza kupata ukweli;
  1. Ninaahidi kushiriki kikamilifu iwapo nitatakiwa katika uchunguzi wowote utakaofanywa na niko tayari kuwajibika iwapo nitakutwa na hatia yeyote.
Napenda niwatoe hofu wananchi wa jimbo la Kigoma Kaskazini walionituma kuja kuwawakilisha hapa Bungeni na Watanzania wote kwa ujumla kwamba:-
  1. Mimi Zitto Zuberi Kabwe sina bei, sijawahi kuwa nayo na sitarajii kuwa nayo huko mbeleni. Daima nimesimamia kidete maadili ya uongozi bora katika maisha yangu yote ya siasa, na nawaahidi sitarudi nyuma katika mapambano dhidi ya rushwa katika nchi hii pamoja na mikakati ya aina hii ya kunidhoofisha na kunivunja moyo;
  1. Nafarijika na salam mbali mbali zinazotolewa kunifariji na kusisitiza kuwa nisilegeze kamba katika mapambano haya, nimepokea ujumbe mwingi kwa simu, sms, tweeter na hata facebook na niko pamoja nanyi Watanzania wenzangu kamwe sitarudi nyuma hadi kieleweke. Naamini katika nchi yetu tunazo rasilimali za kutosha mahitaji/haja ya kila mmoja wetu lakini si ‘tamaa/ulafi’ wa baadhi ya watanzania wenzetu;
  1. Napenda kuweka rekodi sawa kwa Watanzania kwamba nimekuwa Mbunge hiki ni kipindi cha pili, Mimi ni Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) huu ni takriban mwaka wa saba sasa, Kamati yangu inasimamia mashirika 259 ya Umma na si TANESCO peke yake. Mchango wa Kamati hii katika Bunge na kwa ustawi wa Mashirika ya Umma ni bayana na haujawahi kutiliwa shaka. Kamati yetu imeokoa upotevu mkubwa wa mali za umma na kuokoa fedha za umma kutokana na umakini wake. Tumefanya hivyo CHC hivi karibuni, Kiwira na kwenye mashirika mengine mengi. Kote huko uadilifu na uzalendo wa Kamati hii haujawahi kuhojiwa. Inatuwia vigumu kuona kuwa tunahojiwa katika suala hili la TANESCO. Hapa pana kitendawili.
  1. Zipo hoja pandikizi za kutaka Kamati ya POAC ivunjwe na haswa zikinilenga mimi binafsi. Nafahamu kiu ya wasioitakia mema nchi yetu kuiona POAC ikivunjwa au sura zikibadilishwa kwa kuwa Kamati hii imekuwa mwiba kwa mikakati yao ya kifisadi. Kwa maoni yangu, Kamati ya POAC isihusishwe na tuhuma hizi kwa vyovyote vile. Niko tayari nihukumiwe mimi kama mimi na sio kuhusisha wajumbe wengine ambao hawatajwi mahala popote katika tuhuma hizi mbaya sana katika historia ya Bunge letu. Nitakuwa tayari kunusuru Kamati ya POAC na maslahi ya taifa letu kwa kujiuzulu Uenyekiti iwapo itathibitika pasipo shaka kuwa nimehongwa. Kamati ya POAC ni muhimu zaidi kuliko mimi.
  1. Nafahamu pia kuwa kuna wanasiasa hasa wa Upinzani ambao wanautaka sana Uenyekiti wa POAC na wanafanya kila njia kutaka kuidhoofisha. Lakini hawajui kuwa anaepanga wajumbe wa Kamati ni Spika wa Bunge.
  1. Msishangae pia kuja baadae kubaini kwamba baadhi ya wanasiasa wenye midomo mikubwa ya kutuhumu wenzao wao ndio vinara wa kupokea rushwa.
  1. Ni lazima tufike mahali kama viongozi kwamba utaratibu unapokiukwa na yeyote yule, au uongo unapotolewa hadharani tuseme bila kuogopa. Hili ndio jukumu letu kama wabunge na viongozi. Kusimamia ufuatiliaji wa utaratibu ni jukumu letu kama Kamati ya POAC na ndio sababu ya msingi ya kuanzishwa kwa mamlaka kama CAG na PPRA. Haiwezekani, tuwe na set ya kanuni kwa kundi fulani na nyingine kwa makundi mengine, au kuhukumu ufuataji wa taratibu kwa kuangalia sura ya mtu usoni
Mwisho
Kumejengeka tabia hivi sasa ya kuwamaliza wanasiasa wenye kudai uwajibikaji na uzalendo. Kumeanzishwa kiwanda kwenye medani ya siasa cha kuzalisha majungu na fitna zenye lengo la kuwachonganisha wanasiasa wa aina hiyo na wananchi kwa kutumia vyombo vya habari na nguvu ya fedha. Naamini mbinu hizi chafu, kama nyingine nyingi zilizojaribiwa kwangu huko nyuma nazo zitashindwa.
Naamini katika kweli na kweli daima huniweka huru. Naamini kuwa mwale mdogo wa mwanga wa mshumaa hufukuza kiza. Kwa imani hiyo, sitasalimu amri mbele ya dhamira zao ovu hata nitakapobaki peke yangu katika mapambano hayo ya kulinda na kutetea rasilimali za taifa zinufaishe watanzania wote.
Daima nitaongozwa na busara ya Hayati Shabaan Robert isemayo, ‘Msema kweli huchukiwa na marafiki zake, nitakapofikwa na ajali hiyo, sitaona wivu juu ya wale wawezao kudumu na marafiki zao siku zote, siwezi kuikana kweli kwa kuchelea upweke wa kitambo, nikajitenga na furaha ya kweli itakayotokea pale uwongo utakapojitenga”.
Ahsanteni sana.

Zitto Zuberi Kabwe

BRANDY IS BACK NA "PUT IT DOWN" BAADA YA MUDA MREFU.


Mwanadadiva aliyetikisa na ngoma ya Boy is mine akiwa Monica longtime Diva kwenye Brandy amerudi kwa nguvu kwenye kiwanda cha muziki. Mwanzoni mwa Juni alikua akifanya video ya ngoma yake ya “PUT IT DOWN” akiwa amefarnya na Director maarufu duniani Hype Williams akiwa na mwenzake Chriss Brown.
 Alisimama mbele ya Ferrari mbili akionyesha mikogo ya hatari kwa ajili ya video hiyo, ambayo pia kulikuwa na wacheza show wakali Frank Gatson Jr (Beyonce, Kelly Rowland). Mambo kibao atayaweka wazi mwanadada siku zijazo kuhusiana na video yake hiyo ya “CRAZY”. Album yake ya sita itatoka Octoba 2 akiwa amepigwa tafu na Sean Garrett, Bangladesh, Rico Love, Frank Ocean na watu wengine wakali.

ALICIA KEYS KUPERFORM MTV MUSIC AWARDS.


Baada ya kuolewa na kujifungua motto wake wa kwanza, Alicia keys anafuraha sana kwani ataipatia dunia zawadi ya ngoma yake mpya, Mshindi huyo wa Grammy Awards ataperform ngoma yake inayoitwa “CRAZY” akiwa katika stage ya MTV Music Awards Sept. 6 mwaka huu 2012.

No comments:

Post a Comment