Thursday, July 12, 2012


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Meya wa  Manispaa ya Ilala Mhe.Jerry Silaa wakati Meya huyo alipomtembelea na kufanya naye mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo ya Manispaa hiyo. Kiutawala Meya wa Manispaa ya Ilala,ana umuhimu wa aina yake hususani tukizingatia kwamba Ikulu(makazi rasmi ya Rais nchini Tanzania) yapo katika Wilaya ya Ilala. Meya Jerry Slaa,alitumia wakati huo kumkabidhi Rais Kikwete baadhi ya nyaraka muhimu(kama zinavyoonekana mikononi mwa Meya) kuhusiana na masuala hayo hayo ya maendeleo katika Manispaa ya Ilala.
(picha na Freddy Maro)

Read more: BongoCelebrity

No comments:

Post a Comment