Thursday, August 23, 2012
MISS WA LUNDENGA ASHIRIKI SHINDAANO NJE YA NCHI KINYEMELA
Stori: Musa Mateja na Shakoor Jongo
MISS aliyetwaa nafasi ya 2, 2012 katika shindano maalum la mwaka huu, Hamisa Hassan, anadaiwa kuichafua Miss Tanzania kufuatia kwenda kushiriki kinyemela Shindano la Miss University Africa 2012 nchini Nigeria hivi karibuni.
Ilidaiwa kuwa ili mrembo ashiriki shindano hilo, linalopokea walimbwende kutoka barani Afrika, lazima atoke kwenye moja ya vyuo vya nchini mwake sifa ambayo Hamisa hakuwa nayo.
Ilibidi mapaparazi wetu wamsake Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga ‘Anko’ ili atoe ufafanuzi kuhusu madai hayo hasa ikizingatiwa kuwa, katika shindano maalum la hivi karibuni, Lissa Jensen aliibuka kidedea na Hamisa kushika nafasi ya pili.
“Ni kweli Hamisa ni miss wangu, lakini utaratibu wa kwenda Nigeria kushiriki shindano hilo sifahamu aliutoa wapi? Najua hakuna chuo chochote anachosoma kwa sasa na wala hakuna mashindano kama hayo kwangu,” alisema Lundenga.
Kwa upande wake, Hamisa alipobanwa ili kutoa maelezo kuhusu tuhuma hizo alikiri kutosoma chuo chochote nchini.
Aidha, alikiri kushiriki shindano hilo huku akisema kuwa hayupo tayari kuwataja waliomchagua.
“Ni kweli sisomi chuo chochote ingawa nina mpango huo, ni kweli nilikuwa Nigeria kushiriki Miss University Africa 2012 na niliingia top ten, lakini taji lilichukuliwa na mshiriki kutoka Lesotho (pichani chini), lakini siwezi kuwataja walionichagua kwenda,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment