Tuesday, August 21, 2012

DIAMOND KWENYE MKASI


Bila shaka,mojawapo ya kipindi cha Mkasi kilichokuwa kinasubiriwa kwa hamu na wengi ni pamoja na kile kilichorushwa wiki moja iliyopita huku kwenye kiti cha Mkasi akiwa ni Diamond.Zipo sababu nyingi zinazoweza kuwa zimechangia kuamsha hisia hizo; Ni ukweli usiopingika kwamba katika medani ya muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania,Diamond anafanya vizuri sana hivi sasa.Ni wakati wake.Yupo juu(sio mbinguni lakini). Isitoshe,Diamond anaweza kuwa anashikilia rekodi ya mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya ambaye ameandikwa au anaandikwa zaidi na magazeti hususani yale yanayoitwa magazeti pendwa yaani ya udaku.Sababu ni yeye mwenyewe.Ni maisha yake na hadithi zilizomzunguka.
Sasa kama hukupata nafasi ya kukitazama kipindi cha Mkasi cha wiki iliyopita, hiyo hapo chini.Kumbuka tu kwamba,Mkasi huanzia pale Amaya Beauty Salon & Spa mahali ambapo wajanja wote wa mjini hupendezea.Wewe unasubiri nini? Tembelea tovuti ya Amaya na kisha Book Your Appointment.

No comments:

Post a Comment