Kama nilivyoahidi kupitia post hii hapa, Professor Jay(The Heavy Weight MC) ameamua kuingiza mtaani(kupitia kila aina ya media inayoweza kuwafikia wananchi na mashabiki wa muziki) single inayokwenda kwa jina Hellow. Hii inakuwa single ya tatu kutoka katika album ya JaySco Dagama ambayo ingawa bado hajaamua kuitoa rasmi,ni wazi kabisa kwamba pengine itakuwa album bora kabisa kuwahi kutolewa nchini Tanzania na msanii kutoka kizazi kinachoitwa “Kizazi Kipya” au New Generation.
Hellow unatoka katika kipindi muafaka.Kama unafuatilia sindimba za starehe nchini Tanzania,kilichopo kwenye kona ni msimu mnene wa Fiesta.Hellow,bila shaka,inalenga katika kuhakikisha kwamba,mtaani kila mtu anamwambia mwenzake Hellow.
Hii ni production kutoka kwa Dully Sykes ambaye bila shaka utakubaliana nami kwamba ameitendea haki vilivyo chorus ya wimbo huu.Usikilize Hellow
Dk. Steven Ulimboka amerejea leo nchini bna kutyoa shukrani za dhati kwa watanzania kwa dua na michango yao kuinusuru afya yake na kuahidi kuendeleza mapambano dhidi ya huduma bora za afya na maslahi kwa madaktari.
Ulimboka amerejea nchini wakati jamii bado ikiwa katika kizungu mkuti cha nani hasa aliyemteka na kumpa mateso makali Dk. Steven Ulimboka ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini na kiu ya wananchi sasa ni kutaka kujua ukweli kupitia kwake.
Daktari huyo ambaye amejizolea umaarufu nchini kwa harakati za kudai haki na maslahi ya madkatari na huduma bora Hospitalini amerejea leo jijini Dar es Salaam akitokea nchini Afrika kusini ambako alipelekwa na Madaktari wenzake tangu Juni 30 mwaka ambako alikuwa akitibiwa majeraha aliyoyapata baada ya kutekwa na kundi la watu wasiojulikana.
Dk. Ulimboka alitekwa, kupigwa na kutelekezwa kwenye Msitu wa Pande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam ambapo Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaa lilidai kuwa aliyemteka daktari huyo ni raia wa Kenya ambaye tayari wanamshikilia.
Dk. Ulimboka amewasili leo majiya ya saa 8 alasiri katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na SA Airways na kulakiwa kwa shangwe, hoihoi nderemo na vifijo kutoka kwa ndfugu jamaa na marafiki sambamba na madaktari wenzake na wanaharakati.
Hakika Mungu yupo! Na anatenda miujiza yake, Ulimboka inakumbukwa aliondoka nchini akiwa hajiwezi kutokana na hali yake kuwa mbaya na kubebwa katika machela lakini leo amerejea mzima wa afya na anatembea mwenyewe.
Dakika chache zilizopita nimetoka kushuhudia sherehe za kufunga au
kumalizika kwa michuano ya Olympic kwa mwaka 2012 ambayo imekuwa
ikirindima kutoka jijini London nchini Uingereza.
Kama mnavyojua,Tanzania tumeambulia patupu.Ingawa katika michezo siku zote kuna kushinda na kushindwa,kitendo cha Tanzania kutoambulia japo medali moja,kinatia simanzi.Simanzi inazidi pale tunapoona kwamba majirani zetu Kenya na Uganda wao wamerudisha mashujaa wao nyumbani wakiwa na medali ikiwemo ya dhahabu kwa upande wa Uganda.Kwanini sisi tunakuwa wasindikizaji tu?Hivi tunachokiweza sisi ni kipi?Kwanini tuendelee kuwa taifa ya kushindwa tu?Ni maswali mengi na ambayo,bila shaka,yanahitaji majibu ya dhati na sio majibu ya kisiasa kama ambavyo imekuwa ikitokea mara kwa mara.
Lakini wakati tukiambulia patupu,wapo watanzania ambao walijaribu kutuletea kwa karibu kabisa kile kilichokuwa kinaendelea kule London.Hawa ni wakazi wa London.Yupo mtani wangu na mwandishi mahiri,Freddy Macha na pia wapo marafiki zangu wa Urban Pulse.Hizi hapa ni video mbili kutoka kwao.Ya kwanza inazungumzia zaidi siku ya kwanza na ile ya pili ni tathmini juu ya ushiriki wetu.Tizama
Kama mnavyojua,Tanzania tumeambulia patupu.Ingawa katika michezo siku zote kuna kushinda na kushindwa,kitendo cha Tanzania kutoambulia japo medali moja,kinatia simanzi.Simanzi inazidi pale tunapoona kwamba majirani zetu Kenya na Uganda wao wamerudisha mashujaa wao nyumbani wakiwa na medali ikiwemo ya dhahabu kwa upande wa Uganda.Kwanini sisi tunakuwa wasindikizaji tu?Hivi tunachokiweza sisi ni kipi?Kwanini tuendelee kuwa taifa ya kushindwa tu?Ni maswali mengi na ambayo,bila shaka,yanahitaji majibu ya dhati na sio majibu ya kisiasa kama ambavyo imekuwa ikitokea mara kwa mara.
Lakini wakati tukiambulia patupu,wapo watanzania ambao walijaribu kutuletea kwa karibu kabisa kile kilichokuwa kinaendelea kule London.Hawa ni wakazi wa London.Yupo mtani wangu na mwandishi mahiri,Freddy Macha na pia wapo marafiki zangu wa Urban Pulse.Hizi hapa ni video mbili kutoka kwao.Ya kwanza inazungumzia zaidi siku ya kwanza na ile ya pili ni tathmini juu ya ushiriki wetu.Tizama
Professor Jay(jina kamili Joseph Haule) akiwa na majina mengine lukuki kama vile Jay wa Mitulinga,Mr.Red Carpet,Mr.Tough Wallet nk yupo mbioni kuachia single yake inayokwenda kwa jina Hellow ndani ya wiki hii.
Kupitia mtandao wa Facebook,Professor Jay ambaye bado anatingisha anga na vibao lukuki vikiwemo vibao ambavyo amevitoa hivi karibuni kama vile Kama Ipo na KamiliGado,amewataka mashabiki wake ambao wanataka kuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuusikia Hellow ambao amemshirikisha Dully Sykes,kuweka wazi e-mail address zao ili waweze kutumiwa.
Kama upo kwenye Facebook(hivi nani hayupo?) basi wasiliana naye kupitia ukurasa wake au ule wa mashabiki wake ili uwe miongoni mwa wale wa mwanzo kabisa kusikia Hellow.
BC itakuletea kila kitu pia pindi utakapokwenda hewani.
JULIUS Kaisari alipata kutamka; “ My wife ought not even to be under suspicion”- Kwamba mke wangu hapaswi hata kutuhumiwa.
Kaisari alikuwa akijibu swali la kwa nini alimwacha mkewe Pompeia kwa tuhuma za kwenda kinyume na mienendo mema ya ndoa.
Ndio, tuhuma peke yake, hata kabla ya kuthibitishwa, zilitosha kwa Kaisari kumwacha mkewe ili alinde hadhi na heshima yake. Akiamini, kuwa wenye kuhusiana na walio katika uongozi na utumishi wa umma hawapaswi kutuhumiwa kwa kutenda yalo maovu.
Hapa kwetu haijapata kutokea, kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano kuwa kwenye tuhuma nzito ya rushwa kama ilivyo sasa. Ni vema tukatambua sasa uzito wa jambo hili; kwamba kwa Waziri mwenye dhamana kutoa hadharani tuhuma za wabunge kuhongwa ni kashfa kubwa.
Si tu kwa wabunge husika, bali kwa Bunge zima, kwa Serikali nzima, kwa nchi nzima. Hakuna dawa nyingine ya kuondokana na kashfa mbaya kama hiyo isipokuwa kwa wenye kutuhumiwa kukaa pembeni kwa maana ya kujiuzulu ili kupisha uchunguzi wa kina na ripoti yake kwa Bunge na umma.
Maana, hapa kuna mawili yanayotarajiwa kutokea pindi ripoti ya uchunguzi itakapotoka; ama kuwatia hatiani watuhumiwa au kuwasafisha na tuhuma hizo. Hilo la kwanza likitokea ni vema na busara likaendana na hatua kali za kinidhamu na kisheria kwa wahusika hata kama tayari wameshajiuzulu.
Lakini, likitokea la pili, kwamba Tume iliyoundwa kuchunguza kadhia hiyo ikawaona watuhumiwa hawana hatia, hivyo kuwasafisha, basi, Waziri mwenye dhamana aliyetoa tuhuma hizo hadharani na watendaji wenzake wakuu wenye kuhusika na taarifa ya Waziri wanapaswa wajiuzulu mara moja. Ni kwa vile, watakuwa wamesema uongo.
Na hilo ndilo Neno la Leo. ( Hii ni sehemu ya makala yangu kwenye Raia Mwema juma hili)
No comments:
Post a Comment