Saturday, October 7, 2017

SIKILIZA ALICHO KISEMA INDRIS SULTAN KUHUSIANA NA WEMA

https://youtu.be/19rI6RdMswY/

TIZAMA MANENO ALIYO YATOA INDRISI/ DOWNLOAD

Sunday, September 16, 2012

NYIMBO MPYA KUTOKA KWA MR FLAVOR "KWARIKWA"

                                             Nyimbo Mpya Ya Mr Flavour "Kwarikwa"                                  Hii Ndiyo Rmx ya Kwarikwa ya "Mr flavor"

NEW TRACK:DOCHI - IMANI

Tuesday, August 28, 2012

MAPACHA WATATU LEO WAPO COCO BEACH

Bendi ya muziki wa dansi ya MAPACHA WATATU leo jumanne na jumanne zote za kila wiki wanatoa burudani ya kutosha ktk ukumbi wa star coco club uliopo coco beach show hii kali huanza mapema tu saa mbili na nusu usiku..akiongea na bongomic ..meneja wa bendi hiyo KHAMIS DACOTA alisema tumejiandaa vizuri kutoa burudani ya kutosha kwa wadau wa muziki huu sote tukutane coco beach uje ujienjoy na wakali wa muziki wa dansi alimaliza DACOTA

NYOTA TUMAINI LETU.

Jina: AikaRose Mwasha Jinsia:Kike Miaka:12 Utaifa:TANZANIA Mchezo: Taekwando KILO: 28 kg- beginners FEMALE Club: Nong Jang Makazi: Leuven Belgium MAFANIKIO: MEDALI YA FEDHA & DHAHABU Kijana wa kitanzania mwenye ndoto ya kuwakilisha nchi yake kwenye mashindano ya kimataifa hapo usoni kwa kupitia mchezo wa mbinu za kujihami wa TAEKWANDO ,anamapenzi makubwa na mchezo huu aliouanza angali mdogo akiwa na umri wa miaka 9 ,ameshashiriki mashindano madogo madogo nchini Belgium na kupata mafanikio makubwa kufikia medali ya fedha. Hivi karibuni alifanikiwa kupata medali ya dhahabu katika mashindano ya Olympic open Brussels yaliyofanyika Rue Du Lombartzyde Brussels Belgium tarehe 27 May 2012. Sasa hivi anajiandaa na team yake kwenda Copenhagen kwenye mashindano ya Wonderfull Copenhagen yatakayofanyika mwezi ujao. Wito wake hasa kwa vijana wadogo akitilia mkazo jinsia ya kike ni kujifunza michezo mbalimbali na kuwa na ndoto ya kuwa mabalozi kwa taifa lao la TANZANIA. VIPAJI HUINUA TAIFA

Audition ya Maisha Plus 2012 yaanza Awamu ya kwanza ya zoezi la kwasaka vijana watakaoweza kumudu mchakamchaka wa shindano la Maisha Plus, imeanza jana (Agosti 27) huko Bagamoyo mkoani Pwani. Leo shindano hilo litafanya usaili katika wilaya ya Lushoto ambako zoezi hili litafanyika katika maeneo ya mjini mwa wilaya hiyo. Baada ya hapo ratiba za audition zitaendelea kama ifuatavyo; Agosti 29- Kilimanjaro/ Sanya juu Usaili utafanyika katika mji wa Bomang’ombe Agosti 30- Arusha/ Ngorongoro Usaili utafanyika Karatu Agosti 31 – Singida Usaili utafanyika Singida Mjini Septemba 1- Iramba Usaili utafanyika Iramba Mjini Septemba 2- Dodoma Usaili utafanyika Kondoa Mjini Hii ni awamu ya kwanza ya usaili wa shindano hili, audition zitaendelea stay tuned kwaajili ya tarehe na mahali ya auditon zitakazoendelea……….

Thursday, August 23, 2012

MISS WA LUNDENGA ASHIRIKI SHINDAANO NJE YA NCHI KINYEMELA

Stori: Musa Mateja na Shakoor Jongo MISS aliyetwaa nafasi ya 2, 2012 katika shindano maalum la mwaka huu, Hamisa Hassan, anadaiwa kuichafua Miss Tanzania kufuatia kwenda kushiriki kinyemela Shindano la Miss University Africa 2012 nchini Nigeria hivi karibuni. Ilidaiwa kuwa ili mrembo ashiriki shindano hilo, linalopokea walimbwende kutoka barani Afrika, lazima atoke kwenye moja ya vyuo vya nchini mwake sifa ambayo Hamisa hakuwa nayo. Ilibidi mapaparazi wetu wamsake Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga ‘Anko’ ili atoe ufafanuzi kuhusu madai hayo hasa ikizingatiwa kuwa, katika shindano maalum la hivi karibuni, Lissa Jensen aliibuka kidedea na Hamisa kushika nafasi ya pili. “Ni kweli Hamisa ni miss wangu, lakini utaratibu wa kwenda Nigeria kushiriki shindano hilo sifahamu aliutoa wapi? Najua hakuna chuo chochote anachosoma kwa sasa na wala hakuna mashindano kama hayo kwangu,” alisema Lundenga. Kwa upande wake, Hamisa alipobanwa ili kutoa maelezo kuhusu tuhuma hizo alikiri kutosoma chuo chochote nchini. Aidha, alikiri kushiriki shindano hilo huku akisema kuwa hayupo tayari kuwataja waliomchagua. “Ni kweli sisomi chuo chochote ingawa nina mpango huo, ni kweli nilikuwa Nigeria kushiriki Miss University Africa 2012 na niliingia top ten, lakini taji lilichukuliwa na mshiriki kutoka Lesotho (pichani chini), lakini siwezi kuwataja walionichagua kwenda,” alisema.