Just In: Dk.Ulimboka arejea nchini TZ
Kiongozi
wa jumuiya ya madaktari nchini Tanzania, Dk. Steven Ulimboka, akiwa
amebeba maua, na kuzungukwa na Madaktari wenzake na wananchi wa kawaida
waliofika kumlaki, mara alipowasili mapema leo Agosti 12, 2012, kwenye
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
akitokea kwenye matibabu nchini Afrika Kusini. Dk Ulimboka alisema kuwa
yuko fiti na anaweza kufanya shughuli zozote atakazopewa kuanzia sasa.
No comments:
Post a Comment