Thursday, July 12, 2012

GET NEWZ

Mcheza Soka wa Kimataifa,Nazir Khalfan,ambaye yupo nchini baada ya kuitumikia nchi yake katika mchezo kati ya Tanzania(Taifa Stars) na Algeria,hapo jana alipata nafasi ya kumtembelea Rais Jakaya Kikwete katika Ikulu ya Dar-es-salaam ili kumsalimia na kumpa shukrani kwa jinsi ambayo Rais huyo amekuwa mstari wa mbele katika kuendeleza soka nchini.Nazir Khalfan hivi sasa anachezea timu ya Vancouver Whitecaps ya nchini Canada inayoshiriki katika ligi ya Major League Soccer(MLS) ya nchini Marekani na Canada.Mbali na kumshukuru Rais Kikwete,Nazir alimpa zawadi ya jezi yenye jina lake(Kikwete)


Upo uvumi kwamba mchezo wa ngumi za kulipwa ulimwenguni siku hizi umepoteza umaarufu uliokuwa nao tangu enzi za kina Mohamed Ali na kisha enzi za kina Mike Tyson,Lenox Lewis na wengineo. Upande unaopingana na hoja hiyo unadai kwamba wanamasumbwi wa leo kama vile kijana mwenye mbwembwe za aina yake,FLOYD Mayweather Jnr bado ni kivutio kikubwa katika mchezo huo ambao unaaminika kuwa wa pili kwa umaarufu baada ya mchezo wa soka.

Hoja hiyo inaungwa mkono na mshawasha ambao umeshaanza kulipamba pambano linalotarajiwa kupigwa wiki ijayo tarehe 17 Septemba,2011 kati ya Floyd Mayweather na Victor Ortiz

Atapambana na Victor Ortiz kuwania ubingwa wa dunia wa WBC uzani wa welter mjini Las Vegas wiki ijayo.

Pambano hilo litaonyeshwa katika Primetime na Mayweather anatarajia kuweka kibindoni pauni milioni 25 kwa kupitia televisheni hiyo.Je,ni kweli mchezo wa ndondi umepoteza umaarufu?Subiri tuone wikienda.

 
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen leo (Mei 14 mwaka huu) ametangaza kikosi cha wachezaji 25 kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia hatua ya makundi Kanda ya Afrika dhidi ya Ivory Coast.
Akitangaza kikosi hicho ambacho kitaingia kambini kesho kutwa (Mei 16 mwaka huu, Kim amesema uteuzi wake umezingatia uwezo wa mchezaji uwanjani, nafasi anayocheza na ubora wake.
Wachezaji walioitwa ni makipa; Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally (Azam) na Deogratius Munishi (Mtibwa Sugar). Mabeki ni Nassor Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Simba), Waziri Salum (Azam), Shomari Kapombe (Simba) na Juma Nyoso (Simba).
Viungo ni Mwinyi Kazimoto (Simba), Salum Abubakar (Azam), Nurdin Bakari (Yanga), Jonas Mkude (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Edward Christopher (Simba- U20), Mrisho Ngasa (Azam) na Frank Domayo (JKT Ruvu- U20).
Washambuliaji ni Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Ramadhan Singano (Simba-U20), Simon Msuva (Moro United- U20), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Haruna Moshi (Simba) na John Bocco (Azam).
Stars inayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro itacheza mechi ya kirafiki nyumbani Mei 26 mwaka huu dhidi ya Malawi kabla kuivaa Ivory Coast ugenini Juni 2 mwaka huu jijini Abidjan.
Picha na habari kwa hisani ya Father Kidevu



Baada ya kuukosa mwaka jana kwa Dallas Mavericks,hatimaye ndoto ya Miami Heat wakiongozwa na “big three” wao hapo juu, LeBron James, Chris Bosh na Dwayne Wade, imetimia.Usiku huu(alfajiri ya tarehe 22 June kwa saa za Afrika Mashariki),imefanikiwa kunyakua ubingwa wa Ligi ya Mpira wa Kikapu(NBA) nchini Marekani,kwa kuwafunga timu ya Oklahoma City Thunders kwa jumla ya vikapu  121-106 na hivyo kuwatoa Thunders kwa jumla ya michezo 4-1 katika mzunguko wa mechi 7 ambao huwekwa ili kumpata mshindi katika NBA Finals.


aeleweka kwamba mwaka jana Simba walisumbua sana vijana wa Jangwani kiasi hata cha kusababisha Jangwani kuelekea kuparang’anyika kabisa.Sasa mwaka huu Yanga inaaminika wamerudi kwa nia moja tu;kurudisha heshima yao.Je,watakuwa moto wa kuotea mbali au la? Hiki ndicho kikosi kipya cha Yanga




Wachezaji wa Simba (Wabunge) wakishangilia ushindi baada ya kuwafunga watani wao wa Yanga (Wabunge) kwa penalti 3-2.
 
Yanga baada ya kipigo hicho.

Hivi ndivyo hali ilivyokuwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mtanange wa watani wa jadi Simba na Yanga (Wabunge) wakati wa TAMASHA LA MATUMAINI ambapo wabunge wapenzi wa timu ya Simba wameibuka kidedea kwa penalti 3-2. Simba wamefunga penalti 3 wakati Yanga wakifunga 2.




Lauryn Hill, yes,yule yule dada aliyewahi kutamba sana na kundi la The Fugees, anaweza kujikuta akiwa nyuma ya nondo kwa miaka 3.Kisa? Lauryn, kwa miaka karibuni mitatu amekuwa akikwepa kodi au kushindwa kuifahamisha serikali ya Marekani juu ya kiasi cha dola milioni 1.6 alizokuwa ameingiza.Kawaida katika nchi za watu, kila mwaka unatakiwa kuripoti kwamba umeingiza mkwanja wa kiasi gani.Ni sheria.Lauryn hajafanya hivyo kwa miaka 2005,2006 na 2007.
Ms Hill amekiri makosa yake hayo hivi leo huko New Jersey na ingawa mwanasheria wake anasema kwamba Lauryn atalipa kiasi anachodaiwa,bado kuna uwezekano akaenda jela kama adhabu ya kutenda kosa hilo. Wakati wa kusikilizwa kwa shauri hilo,Lauryn aliulizwa kama kuna mtu yeyote aliyesababisha afanye kosa hilo na yeye akasema “sio moja kwa moja,lakini wapo”.
Picha ya Getty Images)


Mwimbaji mwenye sauti ya aina yake na wakati mwingine vituko vya haja,Adele, ametangaza kupitia mtandao wa Popdust kwamba yeye na ubani wake,Simon, wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza kwani hivi sasa yeye ni mjamzito.
Adele ambaye ni mshindi wa tuzo kadhaa za Grammy, amesema yeye na Simon wana furaha kubwa na kwamba alitaka mashabiki wake wapate habari hizo nzuri kutoka kwake mwenyewe lakini pia akaomba fursa ya hadhara iheshimiwe.
Kila la kheri Adele na Simon.Pengine mwanamuziki mwingine ndio anazaliwa!You never know



Kila siku mtandaoni huwa kuna habari ambayo inakuwa kubwa kuliko zingine.Inakuwa gumzo. Leo Alhamisi neno lililozagaa ni kwamba Kanye West ame-tweet picha ya utupu(naked) na mpenzi wake wa sasa,Kim Kardashian.
Picha hiyo inamuonyesha msichana mwenye muonekano unaoshabihiana na Kim Kardashian kwa nyuma akiwa amekaa mahali kama hotelini hivi akionekana kula kitu kama tunda(kama unavyoiona hapo juu). Kwa mtazamo wa kawaida, ilionekana kabisa kwamba huyo ni Kim.Hata hivyo picha hiyo iliondolewa baadae ingawa tayari ilishaingia karibuni kila sehemu ya mtandao.
Swali likabakia ukweli uko wapi? Kwa mujibu wa TMZ, ingawa picha ilisemekana kutoka kwa Kanye West, ukweli ni kwamba ilikuwa ni prank tu ambayo ilianzishwa katika kitu kilichoitwa #WanksterWednesday. Na isitoshe kuna maneno kwamba hata huyo bibie anayeonekana katika picha hiyo sio Kim Kardashian.
ABC News baadae wakatanabaisha kwamba  hiyo ni picha ya muigizaji wa filamu za X anayeitwa Amia Miley na yeye mwenyewe ndio aliwahi ku-tweet hiyo picha yake mwaka jana. Inasemekana Amia Miley anazo picha lukuki zinazomuonyesha akiwa namna hiyo na Kanye West aliwahi kui-tweet katika account yake.
Na mwenyewe Amia Miley amekubali kwamba hiyo picha ni ya kwake na hivyo ndivyo anavyopataga kifungua kinywa chake.
Of course Kanye amekanusha vikali kitu hiki na kukiita kichekesho tu! Kwa hiyo mchezo kwisha.Kanye hana hatia!Nguvu ya Twitter hiyo!

        P SQUARE WAMPOTEZA MAMA YAO

Wasanii wakubwa nchini Nigeria na duniani kote, P-Square wamempoteza mama yao mzazi Mrs Okoye usiku wa kuamkia leo nchini India alipokuwa amepelekwa kwa matibabu baada ya kuhamishwa kutoka katika moja ya hospitali kubwa nchini Nigeria, St Nicholas iliyopo Yaba, Lagos.
inasemekana mama wa wasanii hao, alikua ni moja kati ya nguzo yao kubwa kimuziki kwa kuwapa ushauri na upendo usio na gharama yoyote.
arrangement zinafanyika ili kuurudisha mwili wa marehemu nchini Nigeria.
 
 

TIWA SAVAGE, WIZKID, MABALOZI WAPYA WA PEPSI KUTOKA NAIGERIA

baada ya miezi kadhaa ya maneno ya chini chini, sasa imethibitishwa kuwa wawili hawa ndio mabalozi wapya wa PEPSI. Tiwa Savage na Wizkid walitangazwa usiku wa jana katika exclusive event iliyofanyika Likwid ndani ya Lagos
 
 
 
 

MH ZITO KABWE AKIWA NA WANA KIGOMA ALL STARS


MUONEKANO MPYA WA BARNABA NA MTOTO WAKE STEVEN





huyu ni mtoto wa Barnava aliempa jina la Steven kumuenzi muigizaji wa filamu Tanzania marehemu Steven Kanumba

mama Steve aka wife wa barnaba


BAADA YA KUWAMISS LIKE THREE WEEKS HIVI NOW IM BACK INDA BUILDING FROM LEFT..ADAM, MILLARD & I, ME & MYSELF DJ FETTY.

DIVA LOVENESS LOVE ATAKAENIOA MAHARI SI CHINI YA MILIONI 500


Mwana dadiva anaeendisha kipindi cha ala za roho ndani ya the people's station Diva loveness love jana amefunguka alipokuwa akifanya kipindi cha xxl na mtu mzima Adam Mchomvu kuwa kwa yeyote atakae jitokeza kumuoa basi lazima awe na si chini ya shilingi millioni 500..sikiliza interview hapa chini



   

WASANII WA KIGOMA WATOKA NA NU JOINT LINAITWA LEKA DUTIGITE




Wasanii takribani woote wanaowakilisha mkoa wa Kigoma leo hii wameachia wimbo wa pamoja unaoitwa LEKA DUTIGITE maana yake ni acha tijidai, imetengenezwa na Tuddi Thomas na ndani yake kuna Diamind, Mwasiti, Ommy dimpoz, Linex, Baba Levo, Recho, Peter Msechu, Banana, Makomando na wengineo. sikiliza hapa chini
 
                                                       b

No comments:

Post a Comment