Monday, July 9, 2012

 

 

 

KUMBE KUNA MMILIKI WA JUMBA LA WEMA?

 Siku chache baada ya msanii mwenye vibweka vingi ndani ya tasnia ya filamu Bongo, Wema Abrahamu Sepetu kutangaza kuwa anamiliki mjengo wenye thamani ya shilingi za kibongo Ml 400, hatimaye mmiliki halisi wa mjengo huo ameibuka.

Akizungumza na Teentz.com mapema leo,mmoja watu walio karibu na mmiliki huyo mwenye asili ya kiarabu anayemiliki jina la Ahmed au Msafiri kama anavyojulikana kwenye mitaa hiyo amesema kuwa Wema aliutangazia umma juu ya umiliki wake kwa nyumba hiyo wakati ambao kijana huyo wa kiarabu alikuwa safari nchini Brazil kwenye michongo yake.


“Unajua Wema amewadanya watu kwa kiasi kikubwa, nafikiri anatakiwa kuomba radhi nakuwaeleza ukweli kwenye nyumba ile hana hata kipande cha tofali na mmiliki halisi ni mshikaji wangu Ahmed ambaye mara kadhaa huwa anasafiri kwenda nchini Brail  kibiashara” kilisema chanzo hicho.




for more stories stay with us
……………………………………Stori na Dismas Ten………………………………




Siku tatu baada ya boss wa African Stars Asha Baraka kusema kwamba Max sio Mkurugenzi wa band ya Mashujaa bali ni mpambe tu, Meneja wa band hiyo ambae ni mwezi mmoja toka aihame Twanga Pepeta amemjibu boss wake huyo wa zamani.
Martin amesema “Max sio mpambe wa Mashujaa ni mmoja wa Wakurugenzi wa Mashujaa Investment, sisi hatuna band peke yake… tuna Radio tunataka kuanzisha Lindi, tuna biashara ya magari, Bar na biashara nyingine kwa hiyo Max ni mkurugenzi wa habari pia hivyo huyo anaezungumza kwamba ni Mpambe amechelewa kujua, kumuita mpambe ni kumdhalilisha manake wapambe huwa wanafata fata watu nyuma nyuma ili wapewe shilingi”
Meneja Martin ambae alilipwa milioni 20 kuhamia Mashujaa amesema “tuko kwa ajili ya kuinyanyua band, hii band ndio inaanza na nimekuta ina watu 41, ni wengi sana kwa band inayoanza hata hiyo band ya hao wanaozungumza kwamba tumepunguza watu band yao ina watu 36, kwa hiyo mimi napunguza watu halali wa kufanya kazi na nitaendelea kupunguza manake nataka watu wabaki 28, kikawaida waimbaji kwenye band wanatakiwa wanne lakini hapa nimekuta tisa yani kuna wengine wanakaa mpaka program inakwisha hawajaimba kitu chochote, sio kwamba hawajui kazi ila nilichofanya ni kuwachukuwa wanaojua zaidi kazi''







0

Mpoki ni mchekeshaji wa kundi la Orijino Komedi la TBC 1.

.

.

.

.






















2

Z Anto.
Wote tunafahamu kwamba Z Anto star wa hits kama Binti Kiziwi na Mpenzi Jini, alioa akiwa na umri wa miaka 22 tu tena siku chache baada ya video ya Binti kiziwi ilipotoka ambapo alimuoa mrembo alieuza kwenye hiyo video.
Walikaa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa muda wa mwaka mmoja na kuoana kwenye ndoa ambayo haikumaliza mwaka mmoja, ilivunjika Miaka mitatu iliyopita.
Z Anto anasema “niliamua kumuoa kwa sababu pesa ninazo mali ninazo na nikawa sipendi kuendelea kutenda dhambi, lakini tuliachana kwa sababu ya tamaa zake za kibinaadamu”

Huyu ndio mrembo alieonekana kwenye video ya Binti Kiziwi ambae ndio Z Anto alimuoa na wakaachana baadae.
“Kwa sasa niko tayari kuoa tena manake dini yangu inanilazimisha mimi kuoa, nina mtu ambae bado sijamchumbia na kwa bahati nzuri nimebahatika kupata nae mtoto pia aliezaliwa miezi mitatu iliyopita, plan yangu ni lazima nioe maishani kwa sababu kosa la mtu mmoja haliwezi kunifanya niwaadhibu watu 100, yeye nilimuadhibu na nimeshasahau pia… wakati namuoa alikua na umri wa miaka 20 na mimi nilikua na kati ya 21 au 22″ – Z Anto
0














Jackline Wolper akiwa ameingia uwanjani kwa mbwembwe na kuongea kwa hali ya kutamani pambano lianze mapema apigane na Wema Sepetu, Ulikua ni usiku wa tamasha la matumaini ambapo pambano kati ya Wema na Wolper halikua kama ya mabondia wengine, wao walifanya kama kichekesho ambacho mwisho wa siku walikubali kwamba  mpambano wao ulitumika pia kuwaonyesha watanzania kwamba wawili hao hawana beef.

Ni uwanja wa taifa Dar es salaam july 7 2012.

Wema akiwa anaingia uwanjani kwa mbwembwe nae.

.

.

.

Yani ungekuepo hapa ungecheka tu, kila mtu alikua anacheka.. ilikua safi sana!

Hapa Wema pamoja na mikwara yote aliona J anamletea ngumi yenye ujazo akaamua kukimbia huku akipiga kelele za kutaka aokolewe, mwishowe alikwenda kumkumbatia refa.

Mapumziko.

.

.

Pambano lilikua la round mbili tu ambapo refa alitangaza kwamba wote wametoka droo, hakuna aliemzidi mwenzake kwenye ushindi.

.

.

Baada ya pambano kumalizika huyo jamaa mwenye t shirt nyekundu alikwenda kumshika Wema mapajani akitaka kumbebe ghafla wakati hawajuani na haikua imepangwa hivyo, so jamaa akaambulia kichapo

.

.

Wakati ishu nyingine zikiendelea, Polisi waliibuka walipokaa watazamaji kwenye jukwaa ambalo mara nyingi hutumika namashabiki wa Yanga, hapa kulikua na fujo za kutupiana chupa za maji kutoka kwenye jukwaa la chini na la juu yake, huyo mwenye T shirt nyeusi aliekamatwa na askari ndio anadaiwa kuwa chanzo.

Hao jamaa walilazimika kusimama na kuanza kuwagombeza watu wa jukwaa la juu ambao bado walikua wanaendeleza kurushiana chupa za maji.

Bondia Francis Cheka aligoma kupanda kwenye stage kwa ajili ya pambano na Japhet Kaseba kwa kudai kwamba hawezi kucheza na mtu alie chini ya kiwango, aliyasema hayo pamoja na kwamba alikubali kucheza pambano, hapa kuna utata kidogo… naendelea kuwatafuta wasemaji ili tufahamu taarifa za uhakika.

Pamoja na Japhet Kaseba kutangazwa mshindi kutokana na Cheka kugoma kupanda ulingoni, Cheka alizunguka uwanja kidogo huku akishangiliwa.. Japhet Kaseba wakati anatoka uwanjani kwenda vyumbani mashabiki wa jukwaa la kwanza kushoto mwa lango kuu walimtupia chupa za maji zisizopungua sita pamoja na kumzomea.

.

.

Kija wa EATV, Millard Ayo wa Clouds fm, Maulid Kambaya wa Radio One na Patrick wa EATV.

.

Jose Chameleone wa Uganda alipoanza kuimba, hakwenda kwenye stage.. alizunguka na kuwa karibu zaidi na fans wake.

.

.

.

.

Diamond alimaliza show.

NILIKUA SIJUI KAMA BONGO KUNA HIVI VIPAJI.

Posted: 7th July 2012 by MillardAyo in News
2
Inaweza ikawa sio video imeniteka sanaaa lakini wimbo una nafasi kubwa, nimeukubali… kitu kingine ni swagg za video walizoonyesha wahusika wakuu, Cindy na A.V.I.D ambae kiukweli ana swagg nzuri pia za video na hata kwenye uimbaji, flavour yake ni nyingine kabisa… Cindy nae kaflow vizuri sana kibongo bongo kiukweli nimempa tiki, baada ya kusema hayo yote, naomba utumie dakika zako nne tu kuitazama hiyo video hapo chini….!!!

0

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.
4
Ikiwa ni zaidi ya wiki nne toka Ugomvi ugomvi wa mwimbaji Chris Brown na rapper Drake kutokea kwenye club moja huko New York Marekani, Mtaalamu Mike Rob ameweza kutengeneza VIDEO ya katuni ya jinsi ugomvi wao ulivyotokea kwenye club hiyo.
Mwanzoni mashuhuda walisema chanzo cha ugomvi ni baada ya Chris Brown kujikuta yuko kwenye club moja ya usiku na mtu ambae hawapatani (Drake) na kisa kinadaiwa ni Chris Brown kuhisi Drake anatoka na mpenzi wake wa zamani mwimbaji Rihanna.
Chris baada ya kumuona Drake kwenye club hiyo aliamua kumuagizia kinywaji kama ishara ya kutaka kupatana na kumaliza beef lao ambalo limekua likiendelea kupitia twitter kwa kurudhiana vijembe, baada ya kinywaji kumfikia Drake alikikataa na kummaind Brown na ndipo ugomvi ulipotokea, sasa huyu mtengeneza katuni amepata mkanda mzima wa jinsi ilivyokua na akaweza kutengeneza katuni inavyoonyesha tukio lilivyokua, itazame hiyo video hapo juu.
0

Jaguar mwenye T shirt nyekundu akifanya hiyo video yake mpya ya single inaitwa ‘MATAPELI’  na ni video ambayo wataonekana mastaa kadhaa wa TV Kenya, video inatoka soon.

.

.

.

.

.

Video imefanywa na Ogopa Djs. (Picha zote ni kutoka katika gazeti la Pulse Kenya)








No comments:

Post a Comment