Sunday, July 8, 2012
Jackline Wolper akiwa ameingia uwanjani kwa mbwembwe na kuongea kwa hali ya kutamani pambano lianze mapema apigane na Wema Sepetu, Ulikua ni usiku wa tamasha la matumaini ambapo pambano kati ya Wema na Wolper halikua kama ya mabondia wengine, wao walifanya kama kichekesho ambacho mwisho wa siku walikubali kwamba mpambano wao ulitumika pia kuwaonyesha watanzania kwamba wawili hao hawana beef.
Ni uwanja wa taifa Dar es salaam july 7 2012.
Wema akiwa anaingia uwanjani kwa mbwembwe nae.
.
.
.
Yani ungekuepo hapa ungecheka tu, kila mtu alikua anacheka.. ilikua safi sana!
Hapa Wema pamoja na mikwara yote aliona J anamletea ngumi yenye ujazo akaamua kukimbia huku akipiga kelele za kutaka aokolewe, mwishowe alikwenda kumkumbatia refa.
Mapumziko.
.
.
Pambano lilikua la round mbili tu ambapo refa alitangaza kwamba wote wametoka droo, hakuna aliemzidi mwenzake kwenye ushindi.
.
.
Baada ya pambano kumalizika huyo jamaa mwenye t shirt nyekundu alikwenda kumshika Wema mapajani akitaka kumbebe ghafla wakati hawajuani na haikua imepangwa hivyo, so jamaa akaambulia kichapo
.
.
Wakati ishu nyingine zikiendelea, Polisi waliibuka walipokaa watazamaji kwenye jukwaa ambalo mara nyingi hutumika namashabiki wa Yanga, hapa kulikua na fujo za kutupiana chupa za maji kutoka kwenye jukwaa la chini na la juu yake, huyo mwenye T shirt nyeusi aliekamatwa na askari ndio anadaiwa kuwa chanzo.
Hao jamaa walilazimika kusimama na kuanza kuwagombeza watu wa jukwaa la juu ambao bado walikua wanaendeleza kurushiana chupa za maji.
Bondia Francis Cheka aligoma kupanda kwenye stage kwa ajili ya pambano na Japhet Kaseba kwa kudai kwamba hawezi kucheza na mtu alie chini ya kiwango, aliyasema hayo pamoja na kwamba alikubali kucheza pambano, hapa kuna utata kidogo… naendelea kuwatafuta wasemaji ili tufahamu taarifa za uhakika.
Pamoja na Japhet Kaseba kutangazwa mshindi kutokana na Cheka kugoma kupanda ulingoni, Cheka alizunguka uwanja kidogo huku akishangiliwa.. Japhet Kaseba wakati anatoka uwanjani kwenda vyumbani mashabiki wa jukwaa la kwanza kushoto mwa lango kuu walimtupia chupa za maji zisizopungua sita pamoja na kumzomea.
.
.
Kija wa EATV, Millard Ayo wa Clouds fm, Maulid Kambaya wa Radio One na Patrick wa EATV.
.
Jose Chameleone wa Uganda alipoanza kuimba, hakwenda kwenye stage.. alizunguka na kuwa karibu zaidi na fans wake.
.
.
.
.
Diamond alimaliza show.
NILIKUA SIJUI KAMA BONGO KUNA HIVI VIPAJI.
Posted: 7th July 2012 by MillardAyo in News
0
Inaweza ikawa sio video imeniteka sanaaa lakini wimbo una nafasi kubwa, nimeukubali… kitu kingine ni swagg za video walizoonyesha wahusika wakuu, Cindy na A.V.I.D ambae kiukweli ana swagg nzuri pia za video na hata kwenye uimbaji, flavour yake ni nyingine kabisa… Cindy nae kaflow vizuri sana kibongo bongo kiukweli nimempa tiki, baada ya kusema hayo yote, naomba utumie dakika zako nne tu kuitazama hiyo video hapo chini….!!!
DANNY MRWANDA, PROFESA JAY, DROGBA, KIM KARDASHIAN, MSANJA MKANDAMIZAJI, NTV, GODZILA NA WENGINE.
Posted: 7th July 2012 by MillardAyo in News
0
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
HII NDIO VIDEO YA KATUNI INAYOONYESHA JINSI UGOMVI WA DRAKE NA CHRIS BROWN ULIVYOTOKEA.
Posted: 7th July 2012 by MillardAyo in News
3
Ikiwa ni zaidi ya wiki nne toka Ugomvi ugomvi wa mwimbaji Chris Brown na rapper Drake kutokea kwenye club moja huko New York Marekani, Mtaalamu Mike Rob ameweza kutengeneza VIDEO ya katuni ya jinsi ugomvi wao ulivyotokea kwenye club hiyo.
Mwanzoni mashuhuda walisema chanzo cha ugomvi ni baada ya Chris Brown kujikuta yuko kwenye club moja ya usiku na mtu ambae hawapatani (Drake) na kisa kinadaiwa ni Chris Brown kuhisi Drake anatoka na mpenzi wake wa zamani mwimbaji Rihanna.
Chris baada ya kumuona Drake kwenye club hiyo aliamua kumuagizia kinywaji kama ishara ya kutaka kupatana na kumaliza beef lao ambalo limekua likiendelea kupitia twitter kwa kurudhiana vijembe, baada ya kinywaji kumfikia Drake alikikataa na kummaind Brown na ndipo ugomvi ulipotokea, sasa huyu mtengeneza katuni amepata mkanda mzima wa jinsi ilivyokua na akaweza kutengeneza katuni inavyoonyesha tukio lilivyokua, itazame hiyo video hapo juu.
PICHA 7 ZA UTENGENEZAJI WA VIDEO MPYA YA MSANII JAGUAR WA KENYA.
Posted: 7th July 2012 by MillardAyo in News
0
Jaguar mwenye T shirt nyekundu akifanya hiyo video yake mpya ya single inaitwa ‘MATAPELI’ na ni video ambayo wataonekana mastaa kadhaa wa TV Kenya, video inatoka soon.
.
.
.
.
.
Video imefanywa na Ogopa Djs. (Picha zote ni kutoka katika gazeti la Pulse Kenya)
PICHA 8 ZA WALICHOKIFANYA WEZI KWENYE HILI GARI LA MWIMBAJI KALALA JUNIOUR.
Posted: 7th July 2012 by MillardAyo in News
6
Hili ndio gari la Mwimbaji Kalala Juniour ambae Band yake ya MAPACHA WATATU siku tano zilizopita ilitangaza kuacha kufanya nae kazi.
.
.
.
.
.
Mpaka taa za chini nazo zimeibiwa.
Kalala Juniour na rafiki yake. (Picha zote zimetoka twanga-pepeta.blogspot.com)
JOSE CHAMELEON NDIO HUYU, AMESHATUA BONGO TAYARI KWA SHOW YA LEO! PICHA ZAKE 11 ZIKO HAPA.
Posted: 7th July 2012 by MillardAyo in News
2
Jose Chameleone akiwa Uwanja wa Taifa wa Julius NyerereGarililomleta Chameleone kutoka uwanja wa ndege.
Jose Chameleone ikiwa na Hot wa show ya bongfleva Ray mond mshana
Jose Chameleone
.
Host wa TOTAL REQUEST ya CLOUDS FM Raymond Mshana na Jose Chameleone.
Jose Chameleone na wenyeji wake
Jose Chameleone na DJ wake
Jose Chameleone ndani ya Gari analotumia.
Jose Chameleone ndani ya Gari analotumia kwa siku atakazo kuwa kwenye show
Akiwa anaondoka kwenye mjengo wa CLOUDS FM Mikocheni baada ya kufanya interview.
ASAMOAH GYAN ATANGAZA MAKAZI YA MOJA KWA MOJA.
Posted: 7th July 2012 by MillardAyo in News
1
.
Gazeti la the Sun limeandika line chache na nzito kuhusu maamuzi mapya ya Mchezaji ASAMOAH GYAN ambae amekamilisha uhamisho wake wa moja kwa moja kutoka Sunderland kwenda kucheza soka lake United Arab Emirates akiwa tayari amekipiga kwa mkopo na club hiyo ya Al-Ain kuanzia msimu uliopita.
Mshkaji huyu Mghana alijiunga na Black Cats kutokea Ufaransa kwa ada ya pound milioni 13 mwaka 2010 na alifunga magoli 11 kwenye msimu wake wa kwanza ndani ya English football, pamoja na kufanya uamuzi wa kwenda kucheza U.A.E amesema anajua watu watamkosoa lakini anaifanya kazi yake, alilijadili hilo na familia yake na ikakubali, ni maisha yake.. anachotaka ni kwenda kucheza soka la kiwango.
HII NDIO KAULI YA CHAMA CHA WALIMU KIGOMA KUHUSU MGOMO.
Posted: 7th July 2012 by MillardAyo in News
2
.
Wakati bado ishu ya mgomo wa Madaktari bado iko akilini mwa Watanzania, Chama cha walimu Kigoma kimeonya mwalimu yeyote atakaejaribu kufanya usaliti wa mgomo wao usio na kikomo kwa walimu wote Tanzania unaotarajiwa kuanza siku tatu zijazo.
Katibu wa CWT Kigoma Emmanuel Samara ametoa hiyo tahadhari wakati alipokutana na wawakilishi wa walimu kutoka shule 240 za wilaya ya Kasulu na kuamplfy kwamba katika mgomo wa mwaka 2008 baadhi ya walimu waliwasaliti wenzao na kutoshiriki Mgomo jambo ambalo hawatoliruhusu litokee tena mwaka huu.
Amesema “Mgomo umeitishwa na chama cha wafanyakazi kwa mujibu wa katiba ya chama na walio wengi wameunga mkono, wanachama wetu mashuleni watapiga kura ya kutaka mgomo au kutokutana, hatutaki huu mgomo uwe ni wa chama cha walimu .. uwe ni mgomo wa wafanyakazi wenyewe kwa kuamua kwa kura” – Samara
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment