Saturday, June 23, 2012

News

NANI CHAPAKAZAI KATIKA MZIKI WAKE AKA HARD WORKER?

HUYU NDIO MISS DAR INDIAN OCEAN

mshindi wa miss Dar Indian Ocean Diana Hussein


YANAYOJIRI

Takribani saa 18 tangu alipotamba runingani akimnadi mwanaye kuwa mambo safi, mama mzazi wa Wema Isaac Sepetu, Mariam Sepetu amejificha chumbani baada ya waandishi ‘vichwa ngumu’ kutinga nyumbani kwake wakitaka kufanya naye mahojiano 
Tukio hilo lililokuwa kama filamu ya kivita lilijiri nyumbani kwa mzazi huyo wa Wema, maeneo ya Sinza-Mori, Dar es Salaam Juni 20, mwaka huu, mchana kweupe wakati kukiwa na marudio ya kipindi alichotumia kumnadi mwanaye na kuwananga marafiki zake.
KWA HABARI ZAIDI INGIA http://www.globalpublishers.info

DOGO JANJA AREJEA KWA KISHINDO NDANI YA BONGO




Baada ya mapokezi hayo millardayo.com ilipata nafasi ya kuzungumza Exclusive na Dogo Janja ambae alisema amefurahishwa na hayo mapokezi na kusisitiza kwamba japo aliapa hatorudi kuja kusoma Dar wazazi wake wamemsihi kwamba zile zilikua hasira tu hivyo arudi Dar na aedelee na masomo kitu ambacho amekikubali kwa roho safi.
Janja amesema bado hajasaini mkataba mpya na WATANASHATI lakini kuna watu wake wawili anaowasubiri kwa ajili ya kuja kuupitia pamoja huo mkataba, baada ya hapo ndio atasaini kama amekubaliana nao na atatangaza.
Amesema amebadili mawazo na sasa atasoma Dar es salaam katika shule nzuri ambayo aliahidiwa na Ostaz Juma meneja wa Watanashati, atakua anapelekwa shule na kurudishwa nyumbani kwa gari, anachohitaji pia ni kusoma kwenye shule binafsi nzuri na pia swala lake la muziki kuzingatiwa.
kwenye sentensi nyingine amesema “sasa hivi nitakua naigiza na filamu pia na kina Kitale manake tuko nao kwenye kundi moja la watanashati”
Kwa kumalizia Janja amesema kauli mbiu ya wakati huu imebadilika “kauli mbiu ya wakati nilivyokujaga nilisema nawakalisha matembo sasa hivi nawalaza chali matembo”
HABARI NA MILLAR AYO

MAISHA BORA AU BORA MAISHA KWA KILA MTANZANIA??????



No comments:

Post a Comment